Wafanyabiashara wa matunda katika Soko la Buguruni wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam wameeleza kuwa kwa sasa matunda yanapatikana kwa wingi ,Wachuuzi hao wamebainisha bei ya matunda hayo kulingana na ukubwa na ubora wenyewe.
Wakizungumza leo na Michuzi Tv jijini Dar es Salaam wafanyabiashara hao wamesema kwa sasa hali iko shwari na matunda yanauzika,wateja wao wamekuwa wakipita sokoni hapo kujipatia matuda mbalimbali kuligana na mahitaji yao.
Bei ya machungwa katika soko la Buguruni wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam yanauzwa kati ya sh. 50 hadi 100 kwa bei ya jumla.
Bei ya Nanasi katika Soko la Buguruni linauzwa kati shilingi. 500 hadi shilingi 3500.
Bei ya tikitiki maji ni kati ya Sh 500 hadi Sh. 3000.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
0 Comments