Header Ads Widget

Ticker

6/recent/ticker-posts

Bayport yazindua huduma ya mikopo kwa njia ya mtandao

Msimamizi wa michezo ya kubahatisha kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Mrisho Milao kulia akipata maelekezo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mauzo ya mtandao (Online) wa Bayport Financial Services, Zainabu Kalufya, katika uzinduzi wa huduma mpya ya mikopo ya haraka kwa njia ya mtandao kwa www.kopabayport.co.tz, uzinduzi uliofanyika leo Makao Makuu ya Bayport, jijini Dar es Salaam. Picha kwa Hisani ya Bayport.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
TAASISI ya Kifedhaya Bayport Financial Services, yenye Makao Makuu yake jijini Dar es Salaam, Tanzania, imezindua tovuti yake ya www.kopabayport.co.tz, itakayowezesha wateja wake kupata mikopo ya haraka na kwa njia rahisi.

Kwa kupitia tovuti hiyo, watu mbalimbali wanaweza kupata huduma za Bayport, sanjari na kupata mkopo ndani ya saa 24 baada ya kuidhinishwa, huku akijibiwa ombi lake la mkopo, ndani ya masaa mawili tangu alipojisajiri kwa mara ya kwanza.

Akizungumzia huduma hiyo mpya ya mikopo ya haraka kwa njia ya mtandao jijini Dar es Salaam leo mchana, Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, alisema kwamba huduma hiyo sasa itawawezesha wateja wao kukopa mahala popote atakapokuwa, tofauti na awali.

Baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services kitengo cha Huduma kwa Wateja, wakiwajibika wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya mikopo ya haraka kwa njia ya mtandao onlinewww.kopabayport.co.tz, jijini Dar es Salaam leo.

Post a Comment

0 Comments