Header Ads Widget

Ticker

6/recent/ticker-posts

MAHAFALI YA DARASA LA SABA SHULE YA MSINGI GENIUS KING’S JIJINI DAR

Wahitimu wa darasa la saba Fredrick Robert (kulia) na Rania Hante kutoka shule ya Msingi Genius King’s iliyopo jijini Dar es salaam wakisoma risala yao kwa Mgeni Rasmi Mhandisi Michael Mrema aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo wakati wa mahafali ya nne ya kuwaaga wanafunzi hao iliyofanyika hivi karibuni shuleni hapo.
Mgeni Rasmi Mhandisi Michael Mrema akitoa hotuba kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo wakati wa mahafali ya nne ya kuwaaga wanafunzi wa shule ya Msingi Genius King’s iliyopo jijini Dar es salaam iliyofanyika hivi karibuni shuleni hapo. Waliopo meza kuu ni Wakurugenzi wa shule hiyo, kwanza kulia ni Mkurugenzi Imelda Philip akifuatiwa na Machage Kisyeri. Na wa kwanza kushoto ni Julius Rutabanja.
Wahitimu wa darasa la saba kutoka shule ya Msingi Genius King’s iliyopo jijini Dar es salaam wakiwa katika picha ya pamoja wakiwa wakionesha vyeti mara baada ya kukabidhiwa vyeti hivyo wakati wa mahafali ya nne ya kuwaaga wanafunzi hao iliyofanyika hivi karibuni shuleni hapo.

Post a Comment

0 Comments